Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: kikundi cha kigaidi cha Daesh chafanya janga lingine kwa wananchi wa mji wa Aleppo nchini Syria.
Kikundi hicho cha kagaidi kilifanya tukio hilo la kinyama asubuhi ya siku ya Ijumaa, ambapo walikata maji yanayotumika katika mji wa Aleppo, maji ambayo kituo cha kusafishwa kwake kipo karibu na mto wa furati nchini humo.
Shirika la maji na jumuia ya mwezi mwekundu na baadhi ya taasisi katika mji wa Aleppo bado zinaendelea kufanya juhudi za kutatua tatizo la maji katika mji huo.
Kikundi cha kigaidi cha Daesh siku kadhaa ziliopita pia walikata maji yanayotumika mji mkuu wa Syria Damascus, ambapo mpaka sasa hali mbaya ya kutopatikana maji katika mji huo inaendelea kwa wananchi wa mji mkuu wa Syria.
Kikundi hicho cha kigaidi wameyakata maji hao katika hali ambayo hivi karibuni majeshi ya Syria yamefanikiwa kuukomboa mji wa Aleppo kutoka mikononi mwa magaidi hao, ambapo kimsingi ni pigo kubwa kwa kikundi hicho nchini Syria.
Mpaka sasa mji wa Aleppo uko mikononi mwa majeshi ya Syria, ama magaidi wa Daesh wamekimbilia nje ya mji huo ikiwemo Humeh ya mashariki na kaskazini mwa Aleppo.
mwisho/290
31 Desemba 2016 - 18:24
Msimbo wa Habari: 801946
Kikundi cha kigaid cha Daesh kimezuia maji yanayotumika katika mji wa Aleppo uliopo kaskazini mwa Syria